Xiaoqing Zheng, 59, wa Niskayuna, New York, alitiwa hatiani kwa kula njama ya kufanya ujasusi wa kiuchumi kufuatia kesi ya wiki nne iliyomalizika Machi mwaka jana.
Jaji wa mahakama ya wilaya ya Marekani, Mae D'Agostino pia alimhukumu Zheng kulipa faini ya dola 7,500 na kutumikia mwaka mmoja kuwa chini ya uangalizi baada ya kuachiliwa.
Maafisa wa Marekani wamesema serikali ya China inaleta tishio kubwa zaidi la muda mrefu kwa usalama wa kiuchumi na kitaifa wa Marekani, na inafanya jitihada kubwa kuiba teknolojia muhimu kutoka kwa wafanyabiashara na watafiti wa Marekani. China inakanusha madai hayo.
Facebook Forum