Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:39

El-Nino yasababisha athari kubwa za uhaba wa chakula Somalia


Mtoto mkimbizi wa kisomali akisubiri kufanyiwa uchunguzi wa afya kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya.
Mtoto mkimbizi wa kisomali akisubiri kufanyiwa uchunguzi wa afya kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya.

Mashirika 23 yasiyo ya kiserikali nchini Somalia yanaeleza kwamba nchi hiyo iko kwenye hatari ya kukumbwa na hali ya njaa kama ilivyokuwa 2010 kutokana na ukame na uhaba wa chakula.

Mashirika hayo yametoa taarifa mapema leo yakisema kuwa hali hiyo ni kutokana na hali ya hewa ya El Nino ambayo imejitokeza kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia.

Kulingana na mashirika hayo, athari za El Nino huko pembe ya Afrika zimekuwa mbaya sana, na hivyo kuzidisha changamoto zilizoko za janga la kibinadamu nchini Somalia.

Taarifa hiyo inasema kuwa maelfu ya watu wameathiriwa Somaliland na Puntland huku familia nyingi zikibaki kuwa hoi kutokana na vifo vya mifugo na kupanda kwa gharama za vyakula.

XS
SM
MD
LG