Wanamgambo wa Kiislamu, wenye uhusiano na al-Qaida na kiundi la Islamic State, wamekuwa wakiendesha uasi kaskazini mwa Mali kwa muongo mmoja uliopita.
Askari wa kulinda amani walikuwa kwenye doria ya utafutaji na kugundua mabomu ya Ardhini katika wilaya ya kaskazini ya Tessalit, katika mkoa wa Kidal, wakati waliposhambuliwa , msemaji wa Stephane Dujarric aliwaambia waandishi wa habari.
Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia za walinda amani, kwa wenzetu katika operesheni hii na tunawatakia ahueni ya haraka wale waliojeruhiwa," Dujarric alisema.
MINUSMA -Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kuleta Utulivu wa pande zote nchini Mali kwa sasa una wanajeshi wapatao 12,000 waliotumwa nchini humo.