Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 09:26

Asasi za kiraia Senegal zaungana na upinzani kutayarisha uchaguzi wa Rais


Rais wa Senegal Macky Sall wakati wa mdahalo wa kitaifa huko Diamniadio Februari 26, 2024.
Rais wa Senegal Macky Sall wakati wa mdahalo wa kitaifa huko Diamniadio Februari 26, 2024.

Mungano wa asasi za kiraia nchini Senegal umetangaza kuundwa kwa mungano mpya na vyama vya kisiasa ili kutayarisha uchaguzi wa rais kabla ya tarehe 2 mwezi Aprili.

Katika taarifa yake mungano wa asasi za kiraia Aar Sunu Election, imesema umoja huo mpya utaruhusu kuendeleza hatua na juhudi za pamoja kuzuia juhudi za mapinduzi ya kikatiba yaliyopangwa na serikali.

Kulingana na taarifa hiyo, wagombea 16 kati ya 19 wa upinzani waloidhinishwa na Baraza la Katiba kugombania kiti cha rais katika uchaguzi uloahirishwa Februari 25 wameungana na kuunda umoja unaojulikana kama F24.

Mapema siku ya Alhamisi Rais Mack Sall alithibitisha kuwa ataondoka madarakani ifikapo April 2 na kutangaza kwamba mazungumo ya kitaifa yaliyomalizika Jumatano yamependekeza uchaguzi wa rais wa nchi utafanyika June 2, ikiwa ni miezi miwili baada ya muda wake kumalizika rasmi.

Kituo cha mazowezi cha upigaji kura kilichowekwa na asasi ya Aar Sunu Election mjini Dakar.
Kituo cha mazowezi cha upigaji kura kilichowekwa na asasi ya Aar Sunu Election mjini Dakar.

Siku ya Jumatatu hata hivyo, Sall alionesha ishara za kuweza kubaki hadi uchaguzi kufanyika lakini siku ya Alhamisi alisisitiza kwamba ameshafanya uwamuzi ataondoka na hataki kung’ang’ania madaraka.

Wachambuzi wanasema kutokana na msimamo wa rais wa kuondoka madarakani tarehe 2 April, na uchaguzi kufanyika tarehe 2 June kutakuwepo na changamoto za kisheria kwa kuwa hakutakuwa na mfumo wa uaongozi katika kipindi hicho.

Aar Sunu Election imesema imejipanga na kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo ya kisheria na ndio sababu ya kuharakisha mungano wao.

Forum

XS
SM
MD
LG