Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:12

Asilimia 80 ya fedha zilizoahidiwa kwa ubadilishaji wa nishati Afrika Kusini itakuwa mikopo


FILE PHOTO: South Africa coal miners eye rail investments as crumbling infrastructure depresses exports
FILE PHOTO: South Africa coal miners eye rail investments as crumbling infrastructure depresses exports

Asilimia 80 ya mabilioni ya dola zilizoahidiwa na mataifa tajiri kwa ajili ya kuachana na makaa ya mawe kwa Afrika Kusini itakuwa mikopo,na si ruzuku, na baadhi inaweza kuwa vigumu kuipata kutokana na sheria za kitaifa kulinda kazi za nyumbani, afisa anayefahamu suala hilo aliiambia Reuters.

Takriban asilimia 80 ya mabilioni ya dola zilizoahidiwa na mataifa tajiri kwa ajili ya kuachana na makaa ya mawe kwa Afrika Kusini itakuwa mikopo,na si ruzuku, na baadhi inaweza kuwa vigumu kuipata kutokana na sheria za kitaifa kulinda kazi za nyumbani, afisa anayefahamu suala hilo aliiambia Reuters.

Mwaka jana Marekani, Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ziliazimia kuwekeza dola bilioni 8.5 katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano ili kuisaidia Afrika Kusini kupunguza utoaji wake wa hewa chafu ambayo ni miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa sababu inategemea makaa ya mawe kwa asilimia 80 ya umeme wake.

Mpango huo unakusudiwa kusaidia nchi kupunguza moshi unaochafua na migodi ya makaa ya mawe na kupanga upya maeneo yao kwa paneli za miale ya jua na mashamba ya nishati ya upepo na hatimaye uzalishaji wa magari ya umeme na uzalishaji wa nishati ya hydrojeni.

Hii ingeelekea kufidia nafasi za maelfu ya ajira ambazo zitapotea katika sekta ya makaa ya mawe.

XS
SM
MD
LG