Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:00

Asilimia 50 ya dawa katike kanda ya Afrika magharibi ni ya bandia-UN


aina mbalimbali ya dawa ghushi
aina mbalimbali ya dawa ghushi

Hadi asilimia 50 ya dawa katika kanda ya Afrika magharibi hazikidhi vigezo vinavyostahili au ni ya bandia, Umoja wa mataifa ulionya Jumanne katika ripoti kuhusu biashara haramu ya bidhaa za matibabu.

Biashara hiyo inaweza kusababisha dawa za kuua wadudu kutofanya kazi au maambukizi ya magonjwa hatari, huku pia ikidhoofisha umaanifu katika mifumo ya afya.

Kati ya Januari 2017 na Disemba 2021, takriban tani 605 ya bidhaa za matibabu zilikamatwa huko Afrika magharibi katika operesheni za kimataifa, Ofisi ya Umoja wa mataifa kuhusu dawa za kulevya na uhalifu (UNODC) imesema, ingawa kuna kasoro katika kuripoti kuhusu biashara hiyo haramu na huenda idadi ya dawa hizo ikiwa juu zaidi.

Kote eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, hadi dola milioni 44.7 zinatumiwa kila mwaka kutibu watu waliotumia dawa ghushi za malaria au zisizokidhi vigezo vinavyostahili, ripoti hiyo imesema.

Na hadi vifo 267,000 vinahusishwa kila mwaka na matumizi ya dawa za malaria zisizokidhi vigezo, kulingana na takwim za shirika la afya duniani zilizotajwa na ripoti hiyo.

Mbali na hatari ya bidhaa ghushi na dawa zilizotengenezwa vibaya, ambazo hazifanyi kazi na mbaya zaidi kusababisha maambukizi ya magonjwa hatari, ripoti hiyo imeonya pia juu ya dawa halali kutumiwa kwa njia zisizoidhinishwa.

XS
SM
MD
LG