Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:59

Artur Beterbiev  aendeleza ubabe na kumshinda Yarde kwa KO

Bingwa wa Light Heavy Artur Beterbiev kulia akirusha konde dhidi ya Anthony Yarde huko Wembley Arena, London, Uingereza - Januari 28, 2023 ambapo alimshinda kwa KO. Reuters.
Bingwa wa Light Heavy Artur Beterbiev kulia akirusha konde dhidi ya Anthony Yarde huko Wembley Arena, London, Uingereza - Januari 28, 2023 ambapo alimshinda kwa KO. Reuters.

Bondia bingwa wa Light Heavy wa Canada mwenye asili ya Russia  Artur Beterbiev  amedhihirisha ubabe wake baada ya kumtwanga kwa KO bondia Anthony Yarde wa Uingereza katika raundi ya 8 katika uwanja wa Wembley London Uingereza.

Beterbiev alidumisha rekodi yake ya kushinda kwa KO kwa asilimia 100 na kutetea mataji yake matatu ya uzito wa juu duniani siku ya Jumamosi.

Katika mpambano huo Bertebiev alifikisha rekodi ya mapambano 19-0 yote kwa ushindi wa KO.

Katika mpambano huo Beterbiev alipiga karibu ngumi zake za nguvu, kulingana na CompuBox. Aliunganisha ngumi 84 kati ya 181 za nguvu, kiwango cha asilimia 46.

Akizungumza baada ya mpambano huo mkali Bertebiev alisemakila bondia katika kitengo hiki anaweza kupiga ngumi kali na Anthony anapiga pia ana umri wa miaka 31, ni kijana bado mimi niligeuka kuwa mchezaji wa kulipwa katika umri wa miaka 28, kwa hivyo ana muda bado. Natumai atafanya vyema katika siku zijazo.”

Ushindi huu unaongeza mahitaji kwa bingwa huyu wa WBC, IBF na WBO Artur Beterbiev kuchuana na bingwa wa dunia wa mkanda wa WBA Dmitry Bivol (mwenye rekodi ya 21-0, 11 KO), pia kutoka Russia lakini anayeishi Amerika Kaskazini, ambaye yuko katika kiwango kizuri baada ya kushinda kwa pointi dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez na Gilberto Ramirez mwaka jana.

Hili ndio pambano ambalo linangojewa kwa hamu kubwa.

Yarde (mwenye rekodi ya 23-3, 22 KO) alishindwa kwa mara ya pili katika upiganaji wake na Mrussia aliyepiga sana. Alisimamishwa katika raundi ya 11 katika pambano lake na Sergey Kovalev katika kuwanbia mkanda wa WBO mwaka 2019.

XS
SM
MD
LG