Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:02

Rais Malam Bacai Sanha wa Guinea- Bissau augua


Rais wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha akitoa hotuba katika Umoja wa Mataifa Novemba. 17, 2009.
Rais wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha akitoa hotuba katika Umoja wa Mataifa Novemba. 17, 2009.

Rais wa Guinea Bissau Malam Sinha anatibiwa nchini Senegal

Rais wa Guinea-Bissau Malam Bacai Sanha yuko Senegal kwa matibabu katika mojawapo ya ziara zake nje ya nchi zilizoibua maswali mengi kuhusu hali yake ya afya. Maafisa wa Guinea Bissau wanasema rais Sanha amehamishiwa Dakar, mji mkuu wa Senegal kwa matibabu. Lakini kuna utata juu ya siku aliyopelekwa huko, wengine wakisema ni Jummane wengine Jumatano. Maafisa hao hata hivyo hawakutoa maelezo zaidi juu ya hali yake ya afya. Rais Sanha mwenye umri wa miaka 64 kwa muda mrefu amekuwa na tatizo la kisukari na yasemekana hana damu ya kutosha. Ametafuta matibabu mara kadha nchini Senegal na Ufaransa tangu alipochukua hatamu za uongozi mwezi Septemba mwaka wa 2009. Bwana Sanha alichaguliwa mwezi Julai kuchukua nafasi ya rais Joao Bernado Vieira aliyepigwa risasi na kuuwa mapema mwaka wa 2009.

XS
SM
MD
LG