Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:28

Argentina yatinga nusu fainali ya kombe la dunia


Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi akiwasalimia mashabiki baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Poland katika mechi ya Kundi C ya Kombe la Dunia, Jumatano, Novemba 30, 2022.
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi akiwasalimia mashabiki baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Poland katika mechi ya Kundi C ya Kombe la Dunia, Jumatano, Novemba 30, 2022.

Argentina imefanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga Uholanzi kwa penati 3-2 katika uwanja wa Lusille Doha Qatar.

Kipa wa Argentina, Emiliano Martinez ndiye alikuwa shujaa wa mechi hiyo katika mkwaju wa penalti baada ya timu yake kuruhusu mabao mawili.

Baada ya dakika 120 za jasho na damu timu hizo zilimaliza kwa jumla ya magoli 2-2 baada ya maajabu kufanyika tena katika kombe hili la dunia kutokana na timu ya Uholanzi kurudisha mabao mawili katika ndani ya dakika 7.

Ikiwa ni saa chache tu baada ya Brazil na Neymar kutolewa nje ya michuano hiyo kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Croatia, Argentina ilinusurika na kuibakisha Amerika Kusini kwenye mashindano hayo.

Messi alalamika kuhusu refa akisema “sitaki kuongelea waamuzi maana hapo ndipo watakuwekea vikwazo. Lakini tuliogopa kabla ya mchezo kwa sababu tulijua ni nini kinakuja na Mateu Lahoz hawawezi kumweka mwamuzi kama huyo kwenye mchezo huu wakati hayuko kwenye kiwango” .

Argentina sasa itakumbana na Croatia katika mpambano wa nusu fainali.

Brazil nje Croatia yatinga nusu fainali

Nao Samba Boys Brazil walijikuta wakipata mshangao mkubwa mbele ya mikono ya Croatia baada ya kufungwa kwa penati baada ya dakika 120 za mchezo mkali.

Croatia ambao walikuwa hawapewi nafasi kubwa waliwabana Brazil na kumiliki mpira kati kati na kuhakikisha hakuna mianya kwenye lango lao jambo ambalo timu ya Brazil haijakutana nalo katika mechi za makundi.

Na hatimaye walifanikiwa kuwazuia Brazil kupata bao lolote na kuvunja mpango wao ambao walisema kuwa ilikuwa kufunga mabao ya mapema kama walivyofanya dhidi ya Korea Kusini.

Brazil walipata bao lao la kuongoza katika dakika za nyongeza ikiwa katika dakika ya 106 na ikiwa zimesalia daao hilo kika tatu mchezo kumalizika Bruno Petkovic alisawazisha bao hilo na kupelekea majonzi kwa Brazil ambapo ulimalizika kwa sare ya 1-1 na kuelekea katika penati ambapo walitoka na ushindi wa jumla ya mabao 4-2.

XS
SM
MD
LG