Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 10:49

Argentina yarejesha  matumaini ya kusonga mbele


Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akisherehekea kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Argentina katika uwanja wa Lusail Qatar Novemba 26, 2022 .REUTERS
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akisherehekea kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Argentina katika uwanja wa Lusail Qatar Novemba 26, 2022 .REUTERS

Timu ya taifa ya Argentina hatimaye imefanikiwa kupata ushindi muhimu iliokuwa ikiutafuta baada ya kuwafunga mahasimu wao Mexico kwa bao 2-0 katika uwanja wa Lusail Doha Qatar.

Alikuwa ni Lionell Messi aliyefungua mlango wa Mexico na kuipatia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 64 na kuleta uhai katika timu hiyo wakati zilipokuwa zikishambuliana kwa zamu.

Na kijana Enzo Fernando alimaliza usiku huo kuwa wa raha zaidi kwa Argentina na mchungu kwa Mexico alipopachika bao la pili katika dakika ya 87 na kuhakikishia Argentina ushindi mkubwa waliohitaji katika mechi hiyo.

Hali katika Kundi C hali sasa imebadilika ambapo Poland wanaongoza kundi hilo wakifuatiwa na Argentina na Saudia Arabvia wa tatu huku Mexico wakishika mkia kwa hivyo Saudia Arabia sasa ni lazima washinde mechi yao ya mwisho dhidi ya Mexico ambapo hali ni hivyo hivyo kwa Mexico wanahitaji ushindi kujiweka katika mazingira mazuri.

Enzo Fernandez amefunga goli lake la kwanza la kimataifa kwa Argentina akiwa na umri wa miaka 21.

Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kuingia raundi ya pili kombe la dunia

Bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa imejihakikishia kuingia katika raundi ya pili ya kombe la dunia baada ya kuibwaga Denmark bao 2-1 katika uwanja wa 974 .

Alikuwa ni Kylian Mbappe aliyepachika magoli yote mawili na kuweka rekodi ya kuvunja rekodi ya Thierry Henry wa Ufaransa ya magoli mengi zaidi ya kombe la Dunia.

Mbappe ana umri wa miaka 23 na anakuwa mtu wa pili mwenye magoli mengi zaidi ya kombe la dunia , Pele alifunga jumla ya magoli 7 akiwa na umri wa miaka 24.

Magoli matatu ya Mbappe katika michuano hii ni mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Ufaransa.

Ufaransa watacheza mechi ya mwisho na wawakilishi wa Afrika Tunisia katika uwanja wa Education City siku ya Jumatano.

Australia waipa mshtuko Tunisia

Timu ya taifa ya Australia The Socceroos imeishtua Afrika baada ya kuiangusha timu ya Tunisia kwa bao 1-0 katika uwanja wa Al Janoub Doha Qatar siku ya Jumamosi.

Iliwachukua Australia dakika .kupata bao lao la kuongoza na ushindi kupitia kwa Mitchell Duke kunako dakika ya 23 .

Hivi sasa Australia wanaona mwanga zaidi katika nafasi ya kuingia raundi ya pili ya michuano hii.

Tunisia mpaka sasa hawajashinda mecho yeyotre baada ya kutoka sarae katika mtannage wao wa kwanza na trimu ya Denmark.

Katika kundi hili la D ufaransa ndio vinara wakifuatiwa na Denmark na ili Tunisia waweze kusonga mbele sasa inabidi washinde mchezo wao wa mwisho dhidi ya vinara Ufaransa leu Bleu.

Mashabuki wa Tunisia ambao ni wengi sana mjini Doha kutoka maeneo mengiya nchi Jirani ambao wamesafiri kuja hapa wamepata mshtuko mkubwa baada ya kupoteza mechi hii dhidi ya Australia.

Kwa jumla Kombe la Dunia mwaka huu lina kila aina ya mambo ya kushangaza.

Saudia Arabia yaangushwa na Poland

Timu ya Poland imekata matumaini ya Saudia Arabia na kuiweka katika hali ngumu ya kuingia raundi ya 16 baada ya kuichapa bao 2-0 katika uwanja wa Education City mjini Doha Qatar.

Alikuwa ni mchezaji Zielinski Piotr aliyepachika bao la kwanza kwa Poland kunako dakika ya 38 ya mchezo na Mchezaji mkongwe Robert Lewandowski alipachika msumari wa mwisho kunako dakika ya 82, ya mchezo huo na kupata nafasi ya kufunga goli katika kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Saudia Arabia itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa nafasi nyingi sana katika mchezo huo ikiwa ni Pamoja na kukosa penati.

Kwa maana hiyo ili Saudia Arabia isonge mbele inabidi icheze kufa na kupona katika mchezo wao unaokuja na Mexico.

Lakini Saudia mpaka sasa whawajisikii vibaya kwani wameweka alama katika kombe hili la dunia na Kwa mujibu wa Yahoo News timu hiyo ya w Saudi Arabia imetangaziwa na Mwanamfalme wa Saudia Arabia Mohammed bin Salman Al Saud kuwa kila moja wao atapewa gari aina ya Rolls Royce Phantom kama zawadi ya kitendo hicho cha kihistoria.

Mechi za Jumapili

Siku ya Jumapili timu ya taifa ya Japan Blue Samurai watapambana na Costa Rica waliojeruhiwa vibaya na Uhispania kwa goli 7-0 kwa hiyo wanahitaji kujikomboa.

Nao vijana wa Ubelgiji ambao walishinda mchezo wao wa kwanza wanapamabana na wawakilishi wengie wa Afrika Morocco. Vijana wa Croatia watakumbana na Canada ambao wanahitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wakati Uhispania watapambana na Ujerumani.

Mechi ya Uhispania na Ujerumani pia inasubiriwa kwa hamu ili kuona ni kitu gani Ujerumani watafanya baada ya kujeruhiwa na Japan katika mchezo wao wa kwanza bila kutarajiwa na wengi katika michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia.

Wakati huo huo Brazil itamenyana na Uswisi siku ya Jumatatu bila mchawi wao Neymar, ambaye atakosa kutokana na jeraha la kifundo cha mguu katika ushindi wao wa kwanza wa bao 2-0 dhidi ya Serbia kwenye Kombe la Dunia siku ya Alhamisi, lakini wakiwa na vijana wengi wenye vipaji vya kumsaidia.

Mabingwa hao mara tano wa dunia pia watamkosa pia beki wa pembeni wa kutegemewa Danilo ambaye pia alipata jeraha la kifundo cha mguu dhidi ya Waserbia.

XS
SM
MD
LG