Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 02:50

Chile mabingwa Copa Amerika 2016


Chile wakisherekea ubingwa wa Copa America 2016.

Timu ya taifa ya Chile imechukua tena taji la ubingwa wa Copa Amerika 2016 baada ya kuifunga Argentina mabao 4-2 kwa njia ya penati.

Mchezo huo uliochezwa kwa dakika 120 uliisha katika muda wa kawaida kwa sare ya bila kufungana.

Mpira huo ulioshuhudia refa Heber Roberto Lopes akitoa kadi nyingi ikiwa ni pamoja na kazi mbili za njano kwa Marcelo Diaz ambazo zilipelekea kutolewa nje na nyingine nyekundu kwa Marcos Rojo wa Argentina.

Mpira huo uliisha kwa masikitiko kwa timu ya Argentina baada ya kujikuta wanakosa nafasi nyingine ya kutwaa ubingwa kwani mwaka jana ni timu hizi pia zilicheza fainali.

Na katika mikwaju ya penati Lionel Mesi ambaye alipewa nafasi kubwa ya kufunga mabao alijikuta akiwakosesha raha mashabiki wa nchi yake kwa kukosa penati.

XS
SM
MD
LG