Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa nchi za kiarabu Arab League wamemtaka rais wa Syria Bashar Al Assad kukabidhi madaraka kwa makamu wake wa rais baada ya kuunda serikali ya umoja ikiwa ni hatua ya awali kuitisha uchaguzi wa mapema wa rais na wabunge.
Waziri mkuu wa Qatar Hammad bin Jassim al Thani alitangaza mpango huo jana huko Cairo jana. Inaitaka serikali ya Syria kuanza mazungumzo ya kitaifa na upinzani ndani ya wiki mbili na kwa serikali mpya kuundwa katika miezi miwili.
Al Thani alisema jumuiya ya nchi za kiarabu Arab League itapeleka suala hilo kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa na kuomba uungaji mkono wao.