Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:45

Angola na Ivory Coast zaanza vyema kombe la Afrika


Angola na Ivory Coast zaanza vyema kombe la Afrika

Fainali za kombe la mataifa Afrika zinaendelea katika hatua ya makundi na leo huku kukiwa na mechi mbili kundi C ambapo Gabon inachuana na Niger wakati Morocco inagongana na Tunisia, mechi hizo zote zinafanyika mjini Libreville, Gabon.

Katika mechi za kundi B Jumapili Ivory Coast ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan wakati Angola iliichapa Burkina Faso 2-1 katika mechi zilizochezwa Malabo, Equatorial Guinea. Jumanne Ghana ambao wamewahi kushinda kombe hilo mara nne wanachuana na Botswana katika mechi za kundi D na baadaye Mali dhidi ya Guinea katika kundi hilo.

XS
SM
MD
LG