Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 15:08

Wanaharakati 16 waachiliwa kwa masharti Angola


Mahakama kuu ya Angola imeamuru kuachiliwa kwa masharti kwa wanaharakati 16 wa kisiasa ambao wamekuwa kizuizini kwa kipindi cha miezi 3.

Watu hao ni kutoka kundi la vijana maarufu ‘Luanda Book Club’ waliohukumiwa mwaka uliopita kwa tuhuma za kupanga njama za kupindua serikali ya Rais Eduardo Dos Santos.

Wanaharakati 15 walikamatwa na kuzuiliwa baada ya kuhudhuria mkutano mjini Luanda, Juni 2015.

Wakati wa kukamatwa, wanaharakati hao walisema kuwa mkutano wao ulikuwa wa kujadilia kitabu kilichoandikwa na mwanafilosofia wa Marekani, Gene Sharp, kinachozungumzia mapinduzi ya amani ya tawala kandamizi.

Kuachiliwa kwao kumewashangaza wanaharakati wa kisiasa na haki za kibinadamu ambao wamekuwa wakikosoa serikali ya Angola kwa kukandamiza waandamanaji na pia uhuru wa kujieleza.

XS
SM
MD
LG