Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:46

Angola yawafunga wanaharakati wanne

Ramani ya Angola.
Ramani ya Angola.

Mahakama moja ya Angola imewahukumu kwenda jela wanaharakati wanne wa haki za binadamu kwa uhusiano wao na kundi moja la wanamgambo lililoshutumiwa kuishambulia timu ya mpira wa miguu ya Togo mapema mwaka huu.

Mchungaji mmoja, mwanasheria mmoja na watu wengine wawili kila mmoja alihukumiwa kifungo cha mpaka miaka sita jela Jumanne kwa uhalifu dhidi ya nchi.

Kikosi kamili cha timu ya Togo.
Kikosi kamili cha timu ya Togo.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema madai hayo yalikuwa na ushawishi wa kisiasa, na kuongeza kuwa watu hao hawakuhusika na shambulizi hilo.

Hukumu hiyo imetolewa mwezi mmoja baada ya mkuu wa waasi katika eneo la Cabana lenye utajiri wa mafuta nchini Angola, kusema wanasimamisha uasi wao.

Kundi moja la uasi lililojitenga, linalojulikana kama FLEC lilidai kuhusika kwa shambulizi hilo la kushtukiza kwa timu ya mpira wa miguu kutoka Togo wakati wa michuano iliyofanyika nchini Angola mwezi Januari mwaka huu.

XS
SM
MD
LG