Licha ya kwamba chama kinakabiliwa na uhaba wa fedha na kukosolewa vikali kutokana na ufisadi, uchumi dhaifu, ukosefu wa huduma thabiti ya umeme, kuongezeka kwa uhalifu, utafiti wa maoni unaonyesha kuwa bado chama hicho kina uwezo wa kupata ushindi katika uchaguzi wa bunge wa mwaka huu, utakaoadhimisha miaka 30 tangu kutokomezwa ubaguzi wa rangi nchini humo.
Lakini mzozo huo ndani ya chama na kuenea hali ya kutouamini utawala wa ANC, kunatishia kwa kiasi kukubwa kushuka kwa idadi ya wapiga kura wake na kuleta uwezekano wa kukilazimisha chama hicho kuingia katika makubaliano magumu ya kushirikiana kwenye madaraka na chama kingine.
Zaidi ya hayo yote Rais wa zamani Jacob Zuma ameumaliza mwaka 2023 kwa kuzusha pigo jingine kubwa alipotangaza vita dhidi ya “washirika wake” aliyewaongoza kwa muongo mmoja.
Zuma mwenye umri wa miaka 81, anaekumbwa na kashifa za rushwa, bado ana ushawishi mkubwa—ameapa kufanya kampeni na kukipigia kura chama kipya chenye itikadi kali cha Umkhonto We Sizwe (MK), kilichopewa jina la mrengo wa zamani wa kijeshi wa ANC.
Ingawa anasistiza kubaki katika ANC, Zuma ameilaani serikali ya mrithi wake Rais Cyril Ramaphosa kuwa ya "wasaliti na washirika wa ubaguzi wa rangi."
Ramaphosa alikuwa makamu wa rais wa Zuma lakini hivi sasa ni mahasimu wakubwa, baada ya Zuma kulazimishwa kuondoka madarakani kwa tuhuma za ufisadi mwaka 2018.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum