Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:31

ANC yamuondoa madarakani Malema


Julius Malema kiongozi wa vijana aliyesimamishwa madaraka katika chama tawala nchini Afrika kusini-ANC
Julius Malema kiongozi wa vijana aliyesimamishwa madaraka katika chama tawala nchini Afrika kusini-ANC

Julius Malema kiongozi wa vijana wa chama cha ANC ameondolewa madarakani kuepusha mgawanyiko zaidi katika chama

Chama tawala nchini Afrika kusini-ANC, kimemuondoa kiongozi mwenye utata wa tawi la vijana la chama hicho Julius Malema, baada ya kumkuta na hatia ya kuchochea mgawanyiko na kuharibu sifa za chama.

Kamati ya nidhamu ya ANC kimeamua Alhamisi mjini Johanesburg, kusitisha uwanachama wa Malema kwa miaka 5 kwa utovu wa nidhamu.

Mwenyekiti wa jopo la nidhabu, Derek Hanekom, amesema Malema mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akikiuka maadili ya nidhamu na anaonesha kiburi na kutojali.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mwandishi wa habari wa Radio ya Afrika Kusini, Zabonimpa Abdallah, anasema maoni yamegawanyika miongoni mwa wafuasi wa chama chake kutokana na uwamuzi huo.Tangu achaguliwe kuwa kiongozi wa tawi la vijana la ANC miaka mitatu iliyopita, Malema mara kwa mara ametoa maneno yenye lugha kali hadharani na kukosoa sera za chama chake.

Malema pia alipendekeza kwamba Rais wa zamani nchini humo Thabo Mbeki ni kiongozi bora kuliko Rais wa sasa Jacob Zuma, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa Malema.

Malema alisema Alhamis kwamba atakata rufaa hatua ya chama tawala cha ANC. Msemaji wa chama cha ANC anasema Malema atabaki kwenye orodha ya kulipwa mshahara na chama tawala cha Afrika kusini, akisubiri matokeo ya rufaa yake.

XS
SM
MD
LG