Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:59

Kelly : Amri Mpya ya Katazo la Wahamiaji Itatekelezwa Bila ya Kuleta Vurugu


Waziri John Kelly akiongea kwenye mkutano wa usalama Munich, Ujerumani
Waziri John Kelly akiongea kwenye mkutano wa usalama Munich, Ujerumani

Rais Donald Trump anatarajiwa wiki ijayo kutoa amri ya kiutendaji “itakayo ainisha vizuri zaidi” kukatazwa wahamiaji kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, lakini itatekelezwa vizuri zaidi na pia kuepusha vurugu.

Hii ni katika hatua ya kuepusha zogo lililotokea katika jaribio la kwanza la kuzuia wasafiri wa kigeni waliokuwa wanawasili nchini Marekani, Waziri wa Usalama wa Ndani, John Kelly amesema Jumamosi.

Akizungumza katika Mkutano wa Usalama Munich Ujerumani, unaofanyika kila mwaka, wakati wa jopo la majadiliano kuhusu kupambana na ugaidi, Kelly amesema amri hiyo mpya ya wasafiri haitowazuia wananchi wa kigeni, ambao wana viza za kazi au hati ya makazi ya kudumu-green card, kuingia tena Marekani.

Pia haitowaathiri wasafiri wa kigeni ambao tayari wamewasili katika viwanja vya ndege wakati amri hiyo ikianza kutekelezwa, amesema.

Trump atakuwa amehakikisha kuwa hakuna atakaye zuiliwa katika mfumo huo wa wanaosafiri kutoka nje kuja nchini kupitia viwanja vyetu vya ndege” wakati amri ya kukataza kusafiri ikitekelezwa, amesema Kelly.

Amri hiyo mpya ya uhamiaji inaweza kutolewa mapema Jumanne, habari nchini Marekani zinaeleza hivyo, na Trump mwenyewe amethibitisha hilo kwamba atatoa agizo hizo la kiutendaji wiki ijayo.

XS
SM
MD
LG