Vita vya miezi 15 kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya akiba RSF vinachochewa na usambazaji holela wa silaha nchini Sudan kutoka katika mataifa na mashirika kote ulimwenguni shirika la kutetea haki za binadamu limesema.
Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina la “Silaha Mpya Zinazochochea Migogoro ya Sudan,” imegundua silaha zilizotengenezwa hivi karibuni au kuhamishwa kutoka mataifa kadhaa zikiwemo Russia, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Serbia, Yemen na China zimeingizwa na kutumika katika vita.
Tangu vilipozuka mwezi wa Aprili mwaka jana, vita hivyo vimeua maelfu ya watu, huku wengine wakikadiria idadi ya waliofariki kuwa 150,000, kwa mujibu wa mjumbe wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello.
Forum