Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 05:54

Amnesty: Ukiukaji wa haki umeenea Afrika


Umati wa watu wakikimbia mapigano wakihofia maisha yao kutoka Ivory Coast wakielekea Burkina Faso
Umati wa watu wakikimbia mapigano wakihofia maisha yao kutoka Ivory Coast wakielekea Burkina Faso

Ripoti ya mwaka ya Amnesty International inasema upinzani wa wananchi huko Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini unaonyesha kwamba uhuru wa kujieleza ni msingi wa haki za binadamu.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema katika katika ripoti yake ya mwaka iliyotolewa Ijumaa, kwamba ukiukaji wa haki za binadamu, pamoja na mauaji ya kiholela, mateso yanayofanywa na vikosi vya usalama na marufuku dhidi ya mandamano ya amani, ni mambo ambayo yangali yameenea barani Afrika.

Amnesty inasema mateso yanayofanywa na polisi ni miongoni mwa ukiukaji mkubwa ulioorodheshwa, ikieleza kwamba kesi nyingi za mateso na polisi kutenda maovu zilizoripotiwa Afrika Kusini, mwaka 2010.

Ripoti yake ya mwaka inaeleza kwamba uhuru wa kujieleza ni chombo chenye nguvu cha kuleta mageuzi.

Mkurugenzi wa Amnesty nchini Kenya Julius Nyang'aya anasema nchini Kenya hakukuwa na hatua madhubuti kuwawajibisha wale waliokiuka haki za binadamu wakati wa machafuko ya kisiasa mwaka 2008 nchini humo.

Mkurugenzi wa masuala ya Afrika wa Amnesty Tawanda Hondora anasema haki za kiraia na kisiasa barani humo ziko hatarini.

Nchini Ivory Coast ghasia baada ya uchaguzi wa rais ulokuwa na ugomvi mkubwa mwezi Novemba umesababisha vifo vya mamia ya watu na karibu watu milioni moja kukimbia makazi yao.

Kwingineko Afrika kundi moja la haki za kiraia la Nigeria linasema takriban watu 500 waliuliwa katika ghasia za uchaguzi mwezi Aprili kati ya waislamu na wakristo.

Amnesty inasema mwaka 2010 haukuwa ya habari mbaya pekee. Shirika hilo linasema serikali za Ghana, Nigeria na Kenya zilisitisha mpango wa kuondolewa watu kwa nguvu baada ya malalamiko makubwa ya raia.

XS
SM
MD
LG