Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:36

Amnesty International yashinikiza serikali ya Tanzania kumtendea haki Mbowe


Freeman Mbowe kiongozi wa Chadema akizungumza na waandishi habari katika siku za awali.
Freeman Mbowe kiongozi wa Chadema akizungumza na waandishi habari katika siku za awali.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la  Amnesty Jumatano limesema kwamba mamlaka za Tanzania lazima zitoe mara moja ushahidi wa kuthibitisha mashtaka dhidi ya kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe, au wamwachilie huru, ikiwa siku moja tu kabla ya kufikishwa kwenye  mahakama ya Dar es Salaam.

Mbowe aliyekamatwa Julai 21 wakati akiwa kwenye hoteli moja mjini Mwanza, anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi kati ya mwezi Mei na Agosti 2020. Mbowe alikamatwa wakati akijiandaa kuzindua kongamano la kushinikiza katiba mpya Tanzania.

Muda mfupi baadaye wafuasi kadhaa kutoka chama chake cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) pia walikamatwa lakini kufikia sasa wameachiliwa bila kufunguliwa mashtaka yoyote.

Ripoti zinaongeza kusema kuwa kuna maandamano yaliyopangwa kufanyika leo kupinga kuendelea kushikiliwa kwa kiongozi huyo wa upinzani huku baadhi ya wakosoaji wakisema kuwa ni mwendelezo wa ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Shirika la Amnesty International, Mashariki na Kusini mwa Afrika amesema kuwa ni wakati wa kumuachilia kiongozi huyo mara moja.

-Imetayarishwa na Harrison Kamau, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG