Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:45

Baraza la senate la Marekani kupiga kura mauzo ya bunduki


Watetezi wanounga mkono umiliki wa bunduki Marekani
Watetezi wanounga mkono umiliki wa bunduki Marekani

Wiki moja baada ya shambulizi baya katika klabu moja ya mashoga mjini Orlando Florida kutokea , baraza la senate la Mareknai linatarajiwa kupigia kura mapendekezo kadhaa ya kuzuia uuzaji wa bunduki kwa watuhumiwa wa ugaidi na kuongeza ukaguzi kwa watu wanaonunua bunduki hapa Marekani. Mwandishi wa voa Micheal Bowman ametuandalia ripoti inayoeleza kuwa haiko bayana iwapo hatua za kudhibiti bunduki zinaweza kupita bungeni, ambapo warepublican wengi wnaasema ugaidi unaoshawishiwa na kundi la Islamic State ndio inalaumiwa kwa mauwaji ya Orlando.

Kengele za kanisa zililia huko Orlando wiki moja baada ya Omar Mateen kuanza kufyatuwa risasi katika klabu ya Pulse. Mchana familia zenye kuomboleza , wanazika wapenzi wao.

Seneta wa chama cha demokrat Chris Murphy alisema hatufanyi kitu chochote. Chochote kile. Anasema amechoshwa na mauwaji ya watu wasio na hatia, na amechoshwa na baraza hili kutokuchukuwa hatua.

Wademokrats waliongoza baraza la senate kwa masaa 15 wakidai ipigwe kura dhidi dhidi ya sheria isiyokuwa na nguvu kwa mda mrefu ya kupunguza ghasia za bunduki.

Naye seneta Cory Booker kutoka chama cha Demokrat anasema, imetosha. Imetosha. Imetosha. Hatuwezi kuendelea hivi na kazi kamakawaida katika baraza hili.

Warepublican wanaemdelea kusisitiza kwamba kulenga kudhibiti bunguki siyo mwongozo mzuri.

Wanasema wanahitakji kuwa na mkakati ulio bora ili kuweza kulishinda kundi la ISIS ambalo ndio linashawishi mashambulizi yanayokuwa nchini hapa. Lakini baadae warepublican walikubali upigaji kura ufanyike jumatatu.

Seneta Chris Muphy wa chama cha demokrat anasema tuna nia ya dhati kutoka kwa republican kuwasilisha hatua mbili kwenye baraza la senate kupigiwa kura. Moja ni kuongeza ukaguzi unaofanywa, na pili kuwatowa magaidi katika orodha ya watu wanaoweza kununua bunduki.

Kura pia zinatarajiwa kutoka kwa wareoublican ambazo zinaelezea haki za wamiliki bunduki.

Wafuasi wa haki ya kumiliki bunduki, Marekani.
Wafuasi wa haki ya kumiliki bunduki, Marekani.

Lakini seneta Mrepublican Pat Toomey anasema hatutaki magaidi kuweza kuingia dukani na kununua bunduki. Na hatutaki raia asiye na hatia anayefuata sharia kunyimwa haki zake kwa mujib wa kipengele cha 2 cha katiba kwa sababu yuko kwa bahati mbaya kwenye orodha pamoja na magaidi.

Hatua ya senate juu ya udhibiti wa bunduki haionekani kuwa itafikiwa muafaka wa karibuni na kadhalika katika bunge.

Naye spika wa bunge mrepublican Paul Ryan alisema ,inakwenda baada ya mabadiliko ya kipengele cha pili ni jinsi gani unazuiya ugaidi? La, hio sio njia ya kusitisha ugaidi.

Wiki ilopita huko Orlando, rais alitowa ombi la kuondokana na migawanyiko ya kisiasa.

Rais Obama alisema , niliwakumbatia wanafamila wanaoomboleza na wazazi, na wakauliza kwanini hili linaendelea kufanyika. Na wakaomba tufanye Zaidi kuzuia mauwaji. Hawajali kuhusu siasa.

Wademokrat na warepublican wote wanahofu mashambulizi ya Orlando hayatokuwa ya mauwaji ya mwisho ya watu wengi. Lakini kwa sasa hapo ndipo ushirikiano wa pande mbili unapomalizikia.

XS
SM
MD
LG