Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:37

Wamarekani wakata tamaa kuhusu uhusiano nchini


Waandamanaji mbele ya mahakama kuu ya Marekani mjini Washington
Waandamanaji mbele ya mahakama kuu ya Marekani mjini Washington

Sehemu kubwa ya wamarekani wamekata tamaa kuhusu uhusiano wa watu wa rangi tofuati nchini Marekani.

Kulingana na utafiti uliofanywa na gazeti la Washington Post, asilimia 63 ya wamarekani wanadhani uhusiano kati ya watu wa rangi tofauti uko katika hali mbaya, ongezeko kutoka asilimia 48 iliyopatikana katika utafiti mwingine mapema mwaka huu.

Miongozi mwa wamarekani weusi, asilimia 72 wamekata tamaa kuhusu uhusiano huo.

Mwanandamaji Leshia Evans akikamatwa na polisi hivi karibuni
Mwanandamaji Leshia Evans akikamatwa na polisi hivi karibuni

Ongezeko la hisia hizo kwa kiasi kikubwalinahusishwa na matukio ya hivi karibuni ambako watu weusi waliuawa kwa kupiga risasi na polisi na kuuawa kwa maafisa polisi na mtu mweusi mjini Dallas, Texas.

Wachambuzi wanasema hisia hizo za mgawanyiko katika uhusiano wa baina ya watu wa rangi tofauti huenda ukamfaidisha mgombea urais kutoka chama cha Democratic, Hillary Clinton. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 58 ya wamarekani wanamuamini Clinton kushughulikia swala hilo. Ni asilimia 26 tu ambao wanadhani Mrepublican Donald Trump anaweza kulishughulikia vizuri swala hilo, licha ya matamshi yake kwamba hana hata tone la ubaguzi.

Watu walioshiriki katika utafiti huo wanapendekeza mazungumzo mapana zaidi kuhusu rangi za watu, mageuzi katika mfumo wa sheria za makosa ya jinai, na uongozi bora zaidi kutoka kwa viongozi wa kisaisa.

Naye rais Barack Obama alisema katika hotuba yake ya kila wiki Jumamosi kuwa Amerika ni lazima ianze kuzungumza kwa uwazi zaidi kuhusu tofauti za kirangi nchini humo.

.


XS
SM
MD
LG