Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 06:53

Al-Shabab waua watu 13 kwa mlipuko Mogadishu


Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema mabomu mawili yaliyokuwa kwenye gari ya Al-Shabab yamelipuka nje ya lango la kuingilia uwanja wa ndege wa Mogadishu mapema leo wakati wa asubuhi ambapo kuna shughuli nyingi na kuua watu 13.

Al-Shabab kundi lenye uhusiano na kundi la Al-Qaida zimedai kuhusika na shambulizi hilo kwa mujibu kituo cha redia cha kundi hilo cha Andalus.

Watu 7 kati ya 13 waliouwawa walikuwa walinzi wa Umoja wa Mataifa.

Lango ambalo lililengwa katika shambulizi hilo mara nyingi hutumika na wafanyakazi wa uwanja wa ndege na lipo karibu na majengo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika yanayoungana na uwanja wa ndege.

Wakazi wa endeo hilo wanasema walisikia milipuko mnamo saa tatu asubuhi kwa saa za Somalia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG