Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:23

Al-shabaab wanadai kuhusika na mauji ya Mohamud Qoley


Kundi la Al-Shabaab
Kundi la Al-Shabaab

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limedai kuhusika na mauaji ya ofisa mwandamizi wa upelelezi pamoja na mlinzi wake katika shambulizi la barabarani huko kusini mwa Mogadishu.

Mohamud Moallim Hassan Qoley aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mchana katika wilaya ya Dharkaynlay maafisa walisema. Qoley alikuwa mkuu wa upelelezi katika eneo la Kahda moja ya wilaya 17 katika mji mkuu Mogadishu.

Ofisa huyo alikuwa pamoja na walinzi wawili wakati ufyatuaji ulipotokea kwenye gari ambayo ilikuwa imejificha kwenye uchochoro ambapo mmoja wa walinzi alifariki papo hapo, ofisa huyo alikimbizwa hospitali lakini alifariki alisema Ismail.

Wakati huo huo wanajeshi wane wa serikali waliuwawa baada ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab kushambulia kituo kimoja cha ukaguzi cha jeshi katika mkoa wa Hiran uliopo kaskazini mwa Mogadishu. Maafisa wa eneo waliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba shambulizi lilitokea alfajiri ya Jumapili. Watu wane wengine walijeruhiwa vyanzo vilisema.

Wanamgambo hao walifanikiwa kuchukua silaha kutoka kwa wanajeshi kwenye kituo cha ukaguzi kwenye barabara kuu inayounganisha Somalia na Ethiopia.

XS
SM
MD
LG