Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:39

Al Qaida yauwa wanajeshi 15 Yemen


Eneo lililoshambuliwa katikati mwa Yemen
Eneo lililoshambuliwa katikati mwa Yemen

Taarifa za ndani zinasema kuwa wajumbe wa al- qaida walisimamisha wanajeshi waliokuwa wanaendesha magari ya kiraia kwenye mji wa Ahwar.

Wanamgambo wa Al- qaida kusini mwa Yemen wamefanya shambulizi la ghafla na kuuwa wanajeshi 15 baada ya kusimamisha msafara wao katika jimbo la Abyan.

Taarifa za ndani zinasema kuwa wajumbe wa al- qaida walisimamisha wanajeshi waliokuwa wanaendesha magari ya kiraia kwenye mji wa Ahwar.

Wanamgambo waliamuru wanajeshi kutoka nje ya magari na kuanza kuwapiga risasi katika tukio lililozuka majira ya asubuhi.

Mafia wa ndani wameliambia shirika la habari la kimataifa la reuters kwamba zaidi ya wanajeshi 17 walijeruhiwa lakini inaaminika kuwa bado wanaishi ingawa hawajulikani walipo.

Wakati huo huo Alhamisi kundi la kimataifa la kutetea haki za binadamu lilitoa ripoti likisema kuwa mabomu yaliyotumika katika mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Saudi arabia dhidi ya soko la Yemen yalitolewa na marekani . Takriban watu 100 walikufa katika shambulizi la machi 15.

XS
SM
MD
LG