Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 13:06

Alqaeda wathibitisha kifo cha bin Laden


Osama bin-laden

Kundi la marekani linalofuatilia masuala ya upelelezi SITE lilikariri taarifa inayohusishwa na mtandao huo wa kigaidi .

Al qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake Osama bin Laden .

Kundi la marekani linalofuatilia masuala ya upelelezi SITE lilikariri taarifa inayohusishwa na mtandao huo wa kigaidi na kuonekana kwenye tovuti ya wanamgambo.

Katika taarifa yake alqaeda waliapa kuendelea na mashambulizi yake kwa Marekani na washirika wake ndani na nje ya Marekani. Pia uliahidi kutoa hivi karibuni ujumbe wa sauti ambao wanasema bin Laden alirekodi wiki ile kabla ya kifo chake .

Kwa kuongeza kundi hilo limewataka raia wa Pakistan kupambana dhidi ya serikali yao na na kuisafisha nchi yao kwa kile walichokiita aibu waliyoletewa na kifo cha bin Laden Pakistan.

XS
SM
MD
LG