Ushirikiano wa viongozi wa Afrika katika kupambana na ugonjwa wa mara katika bara la Afrika – Alma, umefungua njia ya kuwezesha nchi za afrika kupambana na ugonjwa huo kwa nguvu moja.
Rais wa Liberia Elen Johnson Sir – Leaf aliyoko ziarani nchini Tanzania ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Alma pamoja na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete aliyemuachia uenyekiti huo leo jijini Dar es salaam wamezindua ofisi za sekretariet ya ushirikiano huo ya viongozi wa Afrika ya kupambana na malaria .
Katika uzinduzi huo rais Kikwete alisema asilimia 89 ya vifo vinavyotokana na malaria duniani kote vinatokea Afrika vivyo akasema ni budi kuunganisha nguvu pamoja ili kutafuta misaada kupambana na ugonjwa huo.
Mwaka 2009 katika mkutano wa umoja wa Afrika viongozi walikubaliana kuanzisha ushirikiano huo.
Kwa mujibu wa marais hao kimsingi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kiwango cha malaria kimepungua kwa asilimia 33 hatua ambayo ni mafanikio kwa chombo hicho.
Hata hivyo rais wa Liberia ametaka asilimia 15 ya kwenye mapato ya nchi hizi kuelekezwa katika sekta ya afya hususan ugonjwa wa malaria kama iliovyoadhimiwa kwenye malengo ya kuadhimishwa ushirikiano huo huko Abuja nchini Nigeria.