Ameuawa katika shambulizi la kombora la kwenye gari huko Gaza.
Israel imesema inachunguza madai kwamba mtu huyo alikuwa mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada la World Kentral kitchen.
Wapalestina 25 wameuawa katika mashambulizi ya makombora ya Israel kote Gaza, usiku wa kuamkia Jumamosi.
Maafisa wa afya wamesema kwamba idadi kubwa ya vifo imetokea sehemu za kaskazini.
Kulingana na shirika la habari la Palestina WAFA, na idara ya ulinzi ya Gaza, kati ya waliouawa ni watu saba, katika shambulizi la Israel dhidi ya nyumba ya makazi ya watu katikati mwa Gaza City.
Idara ya ulinzi ya Gaza imesema kwamba mmoja wa maafisa wake ameuawa katika mashambulizi kaskazini mwa Gaza, sehemu ya Jabalia, na hivyo kufikisha idadi ya maafisa wake waliouawa tangu Okroba 7, 2023 kuwa 88.
Forum