Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:25

Algeria yajianda kupitisha sheria inayominya zaidi uhuru wa vyombo vya habari


Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune

Bunge la Algeria Jumatatu lilikaribia kupitisha sheria inayominya zaidi uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika kaskazini kwa kuweka sheria kali za umiliki wa vyombo vya habari na kuwazuia waandishi wa habari kulinda vyanzo vyao vya habari.

Bunge liliidhinisha mswada huo tarehe 28 Machi na jana Jumatatu Baraza la Seneti lilianza kuujadili, huku kura ikitarajiwa Alhamisi.

Algeria inachukua nafasi ya 134 kati ya nchi 180 katika ripoti ya shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka (Reporters Without Borders) kuhusu uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka wa 2022.

Wakati mswada huo unasema “usiri wa kitaalamu ni haki”, pia utawalazimisha waandishi wa habari kufichua vyanzo vyao hilo likiamriwa na jaji.

Pia watu wenye uraia pacha watazuiliwa kumiliki vyombo vyote vya habari au sehemu ya vyombo hivyo, na waandishi wa habari wanaofanyia kazi vyombo vya habari vya kigeni bila kibali wanaweza kutozwa faini ya karibu dola 7,600.

XS
SM
MD
LG