Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 15:41

Algeria inajenga msikiti mkubwa kukabiliana na wenye msimamo mkali


Wachina vibarua wakifanya kazi mjini Algiers kwenye eneo la ujenzi wa msikiti mkubwa sana barani Afrika.

Ripoti zinasema kwamba Algeria inajenga moja ya msikiti kubwa sana duniani, kwa upande mmoja utakuwa pigo kwa Waislamu wenye msimamo mkali.

Shirika la habari la Ufaransa (AFP) limeripoti kwamba msikiti wa Djamaa El Djazair utajengwa kwenye sehemu iliyo kati ya eneo linaloibuka la kitalii na eneo jingine la makazi ya wafanyakazi wilaya ambayo iliwahi kuwa ngome ya Waislamu wenye msimamo mkali.

Ahmed Madani, ambaye ni mshauri wa waziri wa nyumba anayehusika na ujenzi nchini Algeria, aliiambia AFP kwamba kumekuwa na shutuma kuwa wanajenga hekalu la waislamu wenye msimamo mkali. Alisema kuwa hakuna ukweli wowote kwa shutuma hizo, na kwamba ujenzi wa msikiti huo ni pigo kubwa kwa watu wenye misimamo mikali, ambao ndio wanaopinga mradi huo.

XS
SM
MD
LG