Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Misri, Abdel Fattah al Sisi, ambaye alimuondoa madarakani rais kutoka chama cha Ki-Islam, Mohamed Mursi, anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais mwezi huu na alisema kulikuwepo na majaribio mawili ya kutaka kumuuwa.
Al sisi alisema katika mahojiano ya pamoja na vituo viwili binafsi vya televisheni nchini Misri, cha CBS na ONTV kwamba “kulikuwepo na majaribio mawili ya kuniua . Nina muamini mungu, siogopi”.
Hakusema ni lini majaribio hayo ya kutaka kumuuwa yalitendeka. Al Sisi anatarajiwa kushinda kiurahisi kwenye uchaguzi wa rais wa Mei 26 hadi 27. Mgombea pekee anayeshindana naye ni mwanasiasa mmoja kutoka mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabahi, ambaye alikuwa wa tatu katika uchaguzi wa mwaka 2012 ambapo Mursi alipata ushindi.
Tangu jeshi lilipomuondoa madarakani Mursi mwezi Julai mwaka jana, wanamgambo wameuwa mamia kadhaa ya wanajeshi wa usalama katika mashambulizi ya mabomu na ufyatuaji risasi. Waziri wa mambo ya ndani nchini Misri alinusurika jaribio moja la kuuwawa mwezi Septemba.