Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:17

Al shabab yauwa watu wanane Somalia


Kundi la uokoazi likitoa huduma ya kwanza kwa mtu mmoja kwenye machecha mjini Mogadishu .
Kundi la uokoazi likitoa huduma ya kwanza kwa mtu mmoja kwenye machecha mjini Mogadishu .

Mashahidi wanasema mwanamke mmoja alijilipua mwenyewe wakati waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali akihutubia mkusanyiko wa watu

Kundi la wanamgambo la Al- Shabab limesema limehusika na shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia siku ya jumatano lililouwa watu nane wakiwemo wakuu wa mchezo wa mpira wa soka na Olimpic.

Shambulizi hilo lilitokea katika jumba la michezo lililofunguliwa tena hivi karibuni nchini humo . Mashahidi wanasema mwanamke mmoja alijilipua mwenyewe wakati waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali akihutubia mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiadhimisha mwaka mmoja wa televisheni ya taifa ya Somalia.

Waziri mkuu aliithibitishia VOA kwamba mwanamke huyo alifanya shambulizi na alielezea kuwa hilo ni tukio la kigaidi lililofanywa na Al- Shabab.

Shambulizi hilo limemuuwa mkuu wa kamati ya michezo ya Olimpic Adan Haji Yabarow Wiish na mkuu wa jumuiya ya mchezo wa soka Said Mohamed Nur.

XS
SM
MD
LG