Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 04:06

Al-shabab yashambulia tena makazi ya Rais Somalia


Majeshi ya usalama ya Somalia yakifanya doria nje ya mlango wa Central Hotel, huko Mogadishu, Feb. 20, 2015.
Majeshi ya usalama ya Somalia yakifanya doria nje ya mlango wa Central Hotel, huko Mogadishu, Feb. 20, 2015.

Maafisa wa usalama nchini Somalia wamesema makombora kadhaa yamepigwa Alhamis kwenye makazi ya Rais mjini Mogadishu katika shambulizi moja lililodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Kundi la Al-Shabab lilisema kwamba lilipiga mizunguko kadhaa ambayo ilitua ndani ya eneo la makazi. Haikufahamika mara moja kama shambulizi hilo lilisababisha vifo. Al-Shabab lilidaiwa kuhusika na shambulizi la bomu wiki iliyopita kwenye hoteli moja mjini Mogadishu ambalo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 25 wakiwemo maafisa wawili wa serikali na kumjeruhi Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Kundi la wanamgambo wa Al-shabab
Kundi la wanamgambo wa Al-shabab

Naibu meya wa Mogadishu, Mohamed Aden Guled na mbunge mmoja wa Somalia, Omar Ali Nor walikuwa miongoni mwa waliokufa katika shambulizi hilo la hoteli, maafisa walisema. Miongoni mwa watu 40 waliojeruhiwa walikuwa Naibu Waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Omar Arte na waziri wa usafiri na anga, Ali Ahmed Jama Jangali.

Kundi la al-Shabab limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara yanayolenga serikali na raia nchini Somalia katika miaka ya karibuni kama sehemu ya kile inachosema ni juhudi za kusambaza mtazamo wake wa sheria kali ya ki-Islam.

XS
SM
MD
LG