Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:45

Al-Shabab yadai kuhusika katika shambulizi Mogadishu


Muuguzi akitoa huduma kwa mtu aliyejeruhiwa na shambulizi la Jumanne Mogadishu, Somalia.
Muuguzi akitoa huduma kwa mtu aliyejeruhiwa na shambulizi la Jumanne Mogadishu, Somalia.

Kundi la waislamu wenye siasa kali al-Shabab limedai kuhusika katika shambulizi la bomu liliouwa watu zaidi ya 30 wakiwemo wabunge.

Kundi la waislamu wenye siasa kali Somalia al-Shabab limedai kuhusika katika shambulizi kwenye hoteli moja mjini Mogadishu Jumanne lililouwa zaidi ya watu 30, wakiwemo wabunge sita wa serikali ya mpito.

Msemaji wa al-Shabab, Sheikh Ali Mohamed Rage alitoa tamko la kusema kuwa kundi lao ndio lililohusika katika shambulizi hilo mapema leo.

Mashahidi wameiambia Idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika watu watatu waliokuwa na silaha walishambulia hoteli ya Muna majira ya saa 4 asubuhi kwa saa za Mogadishu.

Wanasema watu hao waliwapiga risasi walinzi wawili nje ya hoteli kabla ya kuvamia ndani na kwenda chumba hadi chumba wakifyatua risasi.

Hoteli hiyo inakaliwa na wabunge wengi wa Somalia na maafisa wa serikali. Mbunge mmoja Hawo Abdullahi Qayad, aliambia VOA washambuliaji wawili walikuwa wamevalia fulana zenye mabomu na walijilipua walipoishiwa na risasi.

XS
SM
MD
LG