Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 04:30

Al-Shabab yaapa kuhamishia vita Kenya


Wanamgambo wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia
Mmoja wa makamanda wa vyeo vya juu katika kundi la al-Shabab la nchini Somalia lenye uhusiano na al-Qaida amesema Alhamis kuwa kundi hilo litahamishia vita vyake nchini Kenya.
“Vita vitahamia Kenya kama wanamuua msichana mmoja wa kisomali, tunamuua msichana mmoja wa Kikenya,“ Fuad Mohamed Khalaf mmoja wa makamanda waandamizi wa kundi la al-Shabab alisema katika matangazo ya kwenye redio moja.

Khalaf alisema katika hotuba iliyotangazwa kwenye redio ya al-Shabab ya Andalus kwamba “tunawasihi waislam wote nchini Kenya kupambana na serikali ya Kenya ndani ya nchi hiyo kwa sababu wakenya waliwauwa watu wako wakiwemo watoto”.

Wanajeshi wa Kenya waliiingia kusini mwa Somalia mwaka 2011 kupambana na kundi la al-Shabab na baadaye walijiunga na jeshi lililopo sasa la wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika chini ya kanuni za Umoja wa Mataifa ili kupambana na waislam wenye msimamo mkali.

Ndege za mapigano zinazoaminika kutoka Kenya zimeshambulia ngome za al-Shabab wiki hii kama sehemu ya msukumo wa karibuni uliofanywa na jeshi la AU dhidi ya waasi.

“Wakati wanajeshi wake na ndege za vita zinawauwa watu wako, Mungu anakuruhusu wewe kulipiza kisasi, tutapambana na wakenya”, Khalifa alisema.

Kundi la al-Shabab ambalo lilidai kuwajibika kwa shambulizi la Septemba mwaka 2013 kwenye eneo lenye maduka mengi la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuwawa, pia limekuwa likilaumiwa kwa mifululizo ya milipuko ya maguruneti na mauaji.

Al-Shabab walisema walikuwa wapiganaji wao waliofanya shambulizi la kushtukiza lililosababisha mauaji na idadi kadhaa ya watu kujeruhiwa wakati Marekani inasema ilikuwa ikijiandaa kupunguza idadi ya wafanyakazi nchini Kenya kwa sababu ya kuongezeka vitisho vya mashambulizi.
XS
SM
MD
LG