Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:09

Al-Shabab watishia kushambulia Burundi


Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imewaonya Wamarekani wasiende Burundi, ikisema kuna vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Somalia-al Shabab.

Marekani imewaonya raia wake wasiende Burundi na kuwashauri wafanyakazi wa serikali ya Marekani walioko nchini humo kuchukua tahadhari haswa nyakati za usiku.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imewaonya raia wote wa Marekani wasiende Burundi, ila kwa shughuli muhimu sana, ikisema kuwa kuna vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Somalia-al Shabab, pamoja na uhalifu wa hali ya juu ndani ya taifa hilo maskini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kundi la al-Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya Burundi na huenda likalenga maslahi ya Marekani.

Onyo hilo linaonya Wamarekani walioko Burundi wasitumie barabara kuu kuanzia jioni hadi alfajiri. Inasema magenge yenye silaha huvizia magari kwenye barabara kuu zinazoingia mji mkuu Bujumbura.

XS
SM
MD
LG