Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:16

Al-Shabab watishia kuishambulia Kenya


Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia.

Kamishna wa polisi nchini Kenya anasema kundi la wanamgambo la al-Shabab linatishia kushambulia viruo vyenye watu wengi nchini Kenya katika siku chache zijazo, wakati wakristo wanaposheherekea sikukuu ya Easter.

Kamishna wa polisi nchini humo, Matthew Iteere, alisema jana Alhamisi kwamba polisi wana taarifa juu ya tukio hilo. Alisema usalama umeongezwa kuzunguka maeneo yanayolengwa ambayo yanajumuisha maduka, sehemu za ibada, sehemu za mapumziko na majengo ya serikali. Iteere hakutaja majina ya miji.

Kundi la Al-Shabab linadai kuhusika na milipuko miwili ya kujitoa mhanga ambayo iliuwa watu 76 nchini Uganda mwezi Julai mwaka jana. Kundi hilo pia lilitishia kufanya mashambulizi nchini Kenya mwezi Februari, baada ya Kenya kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kuwasaka wanamgambo wa kundi hilo.


XS
SM
MD
LG