Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 13:45

Al-shabab bado ni kitisho kwa nchi za AMISOM


Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab la nchini Somalia
Jeshi la Marekani linaamini kuwa kundi la wanamgambo wa ki-Islam la al-Shabab litaendeleza vitisho na mashambulizi yake dhidi ya mataifa ambayo yanachangia wanajeshi wake katika jeshi linaloongozwa na Umoja wa Afrika-AMISOM nchini Somalia.

Kamanda wa AFRICOM, David Rodriguez anasema licha ya ukweli kwamba katika miezi ya karibuni maeneo yanayodhibitiwa na al-Shabab yamepungua lakini kundi hilo linaendelea kuwa kitisho.

“Tunafikiri kwamba wanaendelea kushambulia nchi zinazochangia wanajeshi ili kujaribu kuvuruga na kuwachanganya watu wa nchi hizo hivyo basi uungaji mkono wao katika juhudi za AMISOM ziwe na kidhibiti kutoka mataifa hayo. Hivyo basi kile wanachotaka kukifanya ni kuyaondoa mataifa hayo nchini Somalia na kuwatisha, wanawashambulia katika nchi zao kuonyesha na kuwaeleza watu wa nchi hizo kwamba sio jambo la busara kuendeleza juhudi za kuunga mkono AMISOM”.

Kenya ilishambuliwa tena na kundi la wanamgambo hao Ijumaa wakati mabomu mawili yaliyotegwa kwenye gari yalipolipuka mjini Nairobi na kuwauwa watu 10. Shambulizi hilo lilitokea muda mfupi baada ya nchi kama Uingereza na Marekani kutoa tahadhari ya kusafiri kwenda maeneo kadhaa nchini Kenya kwa sababu ya vitisho vya usalama.

Jenerali Rodriguez anasema wanamgambo wa kundi la al-Shabab bado wanaendelea kuwa kitisho kwa maslahi ya Marekani katika eneo hilo na huko ulaya na limeanza kutoa kitisho cha mashambulizi kwenye ardhi ya Marekani.

Jenerali Rodriguez anasema Marekani inawapa mafunzo wanajeshi wa AMISOM kabla hawajaingia katika ardhi ya Somalia ili kuongeza uwezo wao.

AFRICOM pia ina timu ndogo kwenye makao makuu ya AMISOM kuunga mkono operesheni dhidi ya kundi la al-Shabab.

Mataifa yanayochangia wanajeshi wake kwa AMISOM ni Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia, Djibouti na Sierra Leone.
XS
SM
MD
LG