Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:14

Al-Shabaab wawashambulia KDF huko Somalia


Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lenye makao yake huko Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lenye makao yake huko Somalia.

Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab wamedai kushambulia kituo kimoja cha jeshi la Kenya kilichopo eneo la kusini-magharibi mwa Gedo nchini Somalia siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa habari wa Shabelle kundi la al-Shabaab lilisababisha hasara kubwa dhidi ya wanajeshi wa KDF katika shambulizi hilo katika kijiji cha Fahahdhum huko Gedo.

Katika shambulizi jingine wanamgambo wamefanya shambulizi la papo hapo na kukimbia dhidi ya vikosi vya Kenya vilivyo kwenye kituo cha ukaguzi katika mji wa Hosingow uliopo kwenye mkoa wa Lower Jubba.

Mji wa Hosingow hivi sasa unadhibitiwa na jeshi la Kenya na vikosi vya Jubbaland.

Wanamgambo wa al-Shabaab walisema waliuteka nyara kwa muda mji huo baada ya kuwazidi nguvu wanajeshi wa KDF na Jubbaland wakati wa shambulizi. Lakini hakukuwa na uthibitisho huru kuhusiana na taarifa hizo.

XS
SM
MD
LG