Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:34

Al-Shabaab wafanya shambulizi mpakani Kenya


Wapiganaji wa Al-Shabaab nchini Somalia
Wapiganaji wa Al-Shabaab nchini Somalia

Wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab nchini Somalia wamefanya shambulizi katika mji unaopakana na Kenya mapema Jumatatu, wakazi wa eneo hilo wamesema.

Shambulizi hilo lilianza mapema alfajiri kwa shambulizi lililofanyika katika mji huo kutoka pande zote, wakazi wameripoti.

Wakazi wawili wa mji wa Beled Hawo wamesema kuwa wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kituo cha kijeshi kilomita sita kaskazini mashariki ya mji huo kwa kutumia wapiganaji waliojitoa mhanga.

Watu hao walitumia gari lenye bomu lililofuatiwa na wapiganaji wa ardhini. Vyanzo vya habari vimesema kuwa askari katika kambi hiyo walielekea Kenya.

Shambulizi la pili lililenga kituo cha polisi ndani ya mji wakitumia mbinu hiyo pia, afisa wa uongozi wa zamani katika eneo la Beled Hawo amesema. Pia mapigano makali yameripotiwa katika kituo hicho.

Wakazi wa eneo hilo wamewaona wapiganaji wa al-Shabab katika mitaa ya Beled Hawo na bado milio ya risasi imeendelea kusikika katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG