Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 09:06

Al Shabaab washambulia kambi ya kijeshi Somalia na kuua maafisa saba


Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia

Wapiganaji wa Kiislamu wa al Shabaab, leo Jumanne walivamia kambi ya kijeshi katika sehemu ya kati ya Somalia, walikolazimishwa kuondoka mwaka jana, na kuwaua takriban wanajeshi saba, akiwemo kamanda wa kambi hiyo, afisa mmoja alisema.

Washambuliaji wa kundi hilo, lenye ushirikiano na kundi la kigaidi la al Qaeda, walivamia kituo katika kijiji cha Hawadley kwa kutumia bomu la kujitoa mhanga, la kwenye gari, na kisha kufyatua risasi, Kapteni Aden Nur, afisa wa kijeshi katika mji ulio karibu, aliliambia shirika la habari la Reuters.

"Tuliwatimua al Shaabab. Tulipoteza wanajeshi saba, akiwemo kamanda wetu," Nur aliambia Reuters. Al Shabaab walidai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa, wakisema kuwa limewaua "askari wengi walioasi, pamoja na kamanda wao".

Kambi hiyo iko takriban kilomita 60 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, na ilitwaliwa kutoka kwa udhibiti wa al Shabaab mwezi Oktoba mwaka jana, na vikosi vya serikali, na wanamgambo wa ukoo, wanaoshirikiana na serikali.

XS
SM
MD
LG