Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:49

Ajali ya ndege yaua Raia 10 Wamarekani


Ajli ya ndege illyotokea eneo la msitu mkubwa huko Costa Rica, Jumapili, Disemba 31, 2017.
Ajli ya ndege illyotokea eneo la msitu mkubwa huko Costa Rica, Jumapili, Disemba 31, 2017.

Maafisa wa Costa Rica wanafanya uchunguzi wa ajali ya ndege iliyotokea Jumapili katika eneo lililo na misitu magharibi mwa mji wa San Jose ambayo imeuwa raia 10 wa Marekani na marubani wawili.

Maafisa wanasema ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la Nature Air ililipuka mara tu ilipoanguka na hakuna mtu aliyenusurika.

Familia moja katika eneo la New York imeeleza Wamarekani watano kati ya waliouwawa ni ndugu wa familia moja waliokuwa likizo.

Wametambuliwa kuwa ni wakazi wa Scarsdale, New York mtu na mkewe Bruce na Irene Steinberg na watoto wao watatu.

XS
SM
MD
LG