Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 26, 2025 Local time: 18:51

Ajali ya ndege ya Nigeria yauwa abiria 153


Wananchi wakirusha mabaki ya ndege ya Dana Airlines , katika eneo la makazi ya watu kaskazini mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed Jumapili Juni 3, 2012.
Wananchi wakirusha mabaki ya ndege ya Dana Airlines , katika eneo la makazi ya watu kaskazini mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed Jumapili Juni 3, 2012.

Rais Goodluck Jonathan ametangaza siku 3 za maombolezo baada ya abiria 153 kufariki dunia kwenye ajali ya ndege Lagos.

Maafisa wa Nigeria wanasema abiria wote 153 waliokuwa kwenye ndege ya abiria wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuangukia jengo la makazi mjini Lagos. Rais Goodluck Jonathan ametangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya waathirika na kuamuru uchunguzi wa kina wa janga hilo. Maafisa kutoka idara ya anga ya Nigeria wamesema ndege ya Dana Airlines ilikuwa ikisafiri Jumapili kutoka Abuja kwenda Lagos ilipoangukia jengo la ghorofa mbili kwenye eneo la makazi ya watu wengi na kusababisha majengo mengine kuungua. Yaaminika abiria wote 153 kwenye ndege hiyo wamefariki dunia. Haikujulikana mara moja ikiwa kuna mtu yeyote ardhini aliyeuawa. Shirika la ndege la Dana lina ndege nyingi aina ya Boeing MD-83 ambazo husafirisha abiria kwa saa nzima kutoka Abuja kwenda Lagos.

XS
SM
MD
LG