Ripoti za awali zinaonyesha vifaa vya kutua vya ndege hiyo vilishindwa kufanya kazi wakati ndege hiyo Jeju Air ilipokuwa ikitua katika mji wa Muan, ulioko umbali wa kilomita 290 kusini mwa Seoul. Ndege hiyo ambayo ilikuwa na abiria 181 ilikuwa ikirejea kutoka Bangkok.
Ni moja ya ajali mbaya sana ya usafiri wa anga nchini Korea Kusini.
“Kati ya watu 179 waliofariki, 65 wametambuliwa, “ idara ya zima moto ya Korea Kusini imesema.
Watu wawili, ambao wote ni wahudumu wa ndege, walitolewa kutoka kwenye mabaki wakiwa hai.
Ajali hiyo ya Jumapili ni moja ya ajali mbaya ya usafiri wa anga inayohusisha ndege ya Korea Kusini tangu mwaka 1997, ambapo ndege ya shirika la Korea Air ilianguka huko Guam na kuua zaidi ya watu 200.
Forum