Taarifa zinasema kwamba ndege hiyo ililazimika kubadilisha safari kuelekea Aktau kutokana na tukio la dharura kwa abiria.
Ndege ya shirika la Azerbaijan, Embraer 190 kutoka Baku kuelekea Grozny, imeanguka mapema Jumatano, karibu na uwanja wa ndege wa Aktau.
Maafisa wanasema watu 30 wamefariki na 28 kunusurika.
Ndege hiyo ilishika moto baada ya kuanguka.
Wizara ya maswala ya dharura ya Kazakhstan imesema maafisa wa uokoaji 52 walitumwa katika eneo la ajali kwa ajili ya uokoaji.
Ndege ilikuwa na abiria 62 na wafanyakazi watano.
Shirika la ndege la Azerbaijan limethibitisha tukio hilo na kuahidi taarifa zaidi baadaye. Uchunguzi unaendelea.
Forum