Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 06:05

Ajali iliyohusisha mamia ya magari China yaua mtu moja


Ajali iliyohusisha mamia ya magari China yaua mtu moja
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:38 0:00

Mtu mmoja amekufa nchini China kwenye ajali iliyohusisha mrundikano wa mamia ya magari kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CCTV ambalo pia limeonyesha picha za ajali hiyo iliyofanyika mapema Jumatano.

Picha zilizochukuliwa kwa ndege zimeonyesha mamia ya magari ya kila aina yakiwa wamerundikana kwenye sehemu moja ya barabara kuu ilifunikwa na ukungu. Taarifa zimeongeza kusema kwamba takriban gari 200 zilihisika kwenye ajali hiyo karibu na mji wa Zhenghou, katika jimbo la Henan.

Ukungu mwingi ulijikusanya nyakati za asubuhi kwenye daraja la mto wa Yellow River mjini humo, na kusababisha msongamano mkubwa wa magari uliopelekea ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG