Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:38

Ajali ya meli Madagascar yasababisha vifo vya watu 85

Watu wakiwa wamekusanyika baada ya ajali mbaya ya meli nchini Madagascar
Watu wakiwa wamekusanyika baada ya ajali mbaya ya meli nchini Madagascar

Ajali ya meli katika ufukwe wa Madagascar wiki hii imesababisha vifo vya watu 85, maafisa wa baharini walisema Alhamisi, baada ya kupata miili 21 zaidi hapo jana.

Ajali ya meli katika ufukwe wa Madagascar wiki hii imesababisha vifo vya watu 85, maafisa wa baharini walisema Alhamisi, baada ya kupata miili 21 zaidi hapo jana.

Mamlaka ya baharini ilisema watu 138 walikuwa kwenye meli hiyo yenye urefu wa mita 12 , iliyozama siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa ni 50 pekee waliookolewa. Waliofariki ni pamoja na watoto watano.

Chombo hicho cha mbao, mashua ya mizigo ambayo haikuidhinishwa kubeba abiria, ilikuwa imeondoka katika kijiji cha Antseraka kuelekea Soanierana-Ivongo, takriban kilomita 100 kuelekea kusini.

Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa injini ya chombo hicho ilikuwa na tatizo la kiufundi, kulingana na Adrien Fabrice Ratsimbazafy wa Shirika la River and Maritime Port Agency.

XS
SM
MD
LG