Maendeleo kwenye chanjo ya HIV ndio suala kuu katika mkutano wa dunia wa ukimwi. Mtaalam wa juu wa ukimwi anasema hawezi kusema lini tiba ya HIV na Ukimwi huwenda ikaptiakana, lakini anasema amefurahishwa na maendeleo yake.
Wanasayansi wanaohudhuria mkutano wa 21 wa kimataifa wa Ukimwi mjini Durban Afrika kusini wanasema bado hakuna chanjo ya kuzuia maambukizo ya HIV na ukimwi.
Mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya kimarekani ya afya na magonjwa ya kuambukiza Dr Anthony Fauci, anasema ni vigumu kutabiri pale chanjo dhidi ya HIV na ukimwi itapatikana, lakini anasema anamatumaini kuwa wanakaribia kupata tiba.
Japo hakuna chanjo maalum ambayo imeonyesha matumaini, lakini wanayasayansi wanaendelea kwa dhati na majaribio ya chanjo HVTN 702. Chanjo hio inayofanyiwa majaribio ilitokana na majaribio yalofanywa nchini Thailand miaka michache ilopita na inaonyesha kiwango fulani cha ufanisi. Majaribio ya chanjo hiyo yanategemewa kuanza huko Afrika kusini na katika baadhi ya mataifa mengine ya Afrika baadae mwaka huu, lakini Dr. Fauci anasema itachukuwa mda kabla matokeo kupatikana.