Hatua hiyo inatoa shinikizo kwa kiongozi mkuu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei, kwa kuwa alipokuwa ofisini, Ahmadinejad aliwahi kumkosoa wazi wazi, wakati juhudi zake za kuwania urais 2021 zilizuiliwa na mamlaka.
Kurejea kwa Ahmedinejad kwenye ulingo wa siasa kunakuja wakati kukiwa na mivutano kati ya Iran na mataifa ya Magharibi, kutokana na kuendelezwa kwa program ya nyuklia ya Tehran, kutoa silaha kwa Russia kwenye vita vyake dhidi ya Ukraine, pamoja na misako dhidi ya wakosoaji wake. Kufikia sasa Ahmadinejad ndiye mgombea mashuhuri kujiandikisha kuwania urais.
Akizungmmza muda mfupi baada ya kujiandikisha, ameapa kufanya mashauriano na dunia, wakati pia akiimarisha uhusiano wa kiuchumi na mataifa mengine, iwapo atashinda. Amesema kuwa ,”Matatizo ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kiusalama, yameongezeka kuliko ilivyokuwa 2013,” akiwa na maana ya mwaka ambao aliondoka madarakani.
Forum